Profesa, Salman Dawood al-Sabawi alimuomboea dua shahidi Haniya wakati alipokuwa akifanya ibada ya Hija ndogo, Umrah, kulingana na ripoti ya Press TV.
Taarifa za wanaharakati katika mitandao ya kijamii hasa X zinaonyesha picha za Sabawi akiwa ameshikilia bendera ndani ya eneo la Masjid al-Haram, eneo takatifu zaidi katika Uislamu. Bango lilisomeka, "Naizawadia Umra yangu hii kwa shahidi Ismail Haniya" kwa Kiarabu.
3489388
Kufuatia habari za kuzuiliwa kwa Sabawi, watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii waliingia kwenye X, Facebook, na majukwaa mengine, wakitaka aachiliwe mara moja na bila masharti. Sabawi ni mkazi wa mji wa Mosul, kusini mwa Iraq.
Ismail Haniya, ambaye alikuwa Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian, aliuawa shahidi pamoja na mlinzi wake katika shambulio la Israel mapema Julai 31.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei ameuonya utawala wa Israel kuhusu "jibu kali" kwa mauaji ya Haniya na kusema kuwa ni jukumu la Jamhuri ya Kiislamu ya kulipiza kisasi damu ya kiongozi wa mapambano ya Palestina.
"Utawala wa Kizayuni wa jinai na kigaidi ulimuua shahidi mgeni wetu mpendwa katika nchi yetu na kutuacha tukiwa tumefiwa, lakini pia ulijiwekea uwanja wa adhabu kali," amesema Kiongozi Muadhamu.